Natumaini kuwa sote ni wazima wa afya
Bila kupoteza muda, niende moja kwa moja kwenye mada. Mimi ni mtaalamu wa Microsoft Excel, Leo nimekuja na template ambayo kazi yake ni kuchakata matokeo ya wanafunzi wa O-Level.
Hii template ina uwezo wa kuchukua wanafunzi 400 na ina worksheets tano, kila worksheet ina kazi yake, nitazielezea moja moja.
1. Worksheet 1 (setting)
Hii ni worksheet ambayo mwalimu atakuwa anafanya setting za grades, divisions n.k
Mfumo wa penalty nimeuweka kama optional, mwalimu atachagua YES/NO kulingana na mahitaji yake.
Wanafunzi ambao watapigwa penalty ni wale ambao watakuwa wamepata division one na division two lakini wamefeli somo la Basic Mathematics au Kiswahili.
Pia katika hii worksheet kuna sehemu mwalimu ataset alama ya ufaulu (pass mark) ambayo itakuwa inalinganishwa na wastani alioupata mwanafunzi kwa masomo saba aliyofaulu zaidi, nitaielezea vizuri dhumuni la kuweka hii passmark katika worksheet inayofuata.
2. Worksheet 2 ( Score sheet )
Hii ni worksheet ambayo mwalimu atakuwa anajaza majina pamoja na alama (marks) za wanafunzi wake. Mwalimu atajaza alama tu, grades zitajijaza zenyewe kulingana na setting ulizofanya kwenye worksheet 1.
Pia mwalimu atajaza jina la shule yake , tarehe, na kidato (Haya maelezo yatatumika katika worksheet zingine).
Worksheet hii itamsaidia mwalimu kuwajua wanafunzi waliofaulu (Pass), wanafunzi waliofeli (Fail), wanafunzi ambayo wamefanya mitihani nusu (chini ya masomo saba, Incomplete) na wanafunzi ambao hawajafanya kabisa mitihani (Absentees).
Wanafunzi wote ambao watakuwa wamevuka alama ya ufaulu (pass mark) ambayo uliijaza kwenye setting watakuwa na highlight nyeupe, wanafunzi ambao watakuwa hawajafikisha alama ya ufaulu watakuwa na highlight ya kijivu(grey), wanafunzi ambao watakuwa wamefanya mitihani ambayo idadi yake haifiki saba watakuwa na highlight ya kijani mpauko, na wale ambao hawajafanya kabisa mitihani watakuwa na highlight ya orange mpauko.
NB: Nimeweka key za highlights zote hapo juu
3. Worksheet 3 (Student's Report)
Hii ni worksheet ambayo kazi yake ni kutengeneza report za wanafunzi wote ambao mwalimu aliwaandika kwenye sheet ya kurekodi marks (score sheet).
Inaonesha nafasi (position) kwa kila mwanafunzi utakayemchagua kwenye list (drop down list, ambayo itadisplay pale utakaposelect cell yenye jina la mwanafunzi)
Worksheet hii mwalimu haruhusiwi kuandika chochote zaidi ya kuchagua jina la mwanafunzi tu, cells zote zilizopo kwenye hii worksheet zinajijaza zenyewe na pia nimezilock ili kulinda formula nilizoziandika.
4. Worksheet 4 (Overall results)
Hii ni worksheet ambayo inaonyesha matokeo ya jumla kwa wanafunzi wote.
Kurasa moja inachukua idadi ya wanafunzi 40, kama idadi ya wanafunzi wako itakuwa ni zaidi ya 40 utachagua page inayofata ili kupata orodha ya wanafunzi wengine (41 mpaka 80) na kuendelea.
5. Worksheet 5 (Results summary)
Hii worksheet inafanya kazi zifuatazo
(i) Inaonesha idadi ya wanafunzi wote waliofanya mtihani (total candidates), na wale ambao hawakufanya (absentees)
(ii) Inaonesha idadi ya madaraja (Divisions)
(iii) Inaonesha asilimia ya wanafunzi waliofaulu na waliofeli
(iv) Inaonesha idadi ya wanafunzi waliofaulu na waliofeli kwa jinsia zote mbili
(v) Inaonesha idadi ya grades kwa masomo yote 11
(vi) Inaonesha idadi ya wanafunzi ambao hawajafanya mtihani wa somo husika kwa masomo yote.
(vii) Inaonesha majina ya wanafunzi bora (top ten) bila kujali nafasi ya mwanafunzi katika orodha. Hata kama mwanafunzi bora jina lake lipo kwenye s/n ya 400, template itamtafuta alipo na kumuweka kwenye nafasi anayostahili.
Worksheet hii mwalimu haruhusiwi kuandika kitu chochote zaidi ya kuprint tu. Cells zote zina formula na zinajijaza zenyewe.
Angalia video hapo chini namna template inavyofanya kazi
TEMPLATE REQUIREMENT
>>> Microsoft Office 2010 na kuendelea, Ms 2007 kuna baadhi ya functions hazipo
Bei ya hii template ni Tsh 35,000/=
Njuka II
Expert in Microsoft Excel
Email: ebusiness.excel@gmail.com
Dar es salaam,
Sunday, 01 November 2020
This comment has been removed by a blog administrator.
ReplyDeleteSawa ndugu, nakupigia
DeleteAu nitumie namba yako tuwasiliane
ReplyDelete